Tuesday, October 22, 2013
WANAWAKE WENGI HUPENDA WANAUME WAPOLE KWA SABABU HII
Tuesday, October 22, 2013 by Unknown
Ukimuuliza binti yeyote mwenye ndoto ya kuolewa,,akutajie sifa za mume ampendae,sifa ya "awe mpole" itakuwa ktk orodha ya mwanzo kabisa.Ktk utafiti binafsi sifa hii imetajwa na wasichana 74 ikiwa ya kwanza,,wasichana 113 ikiwa ya 2.Lakini kwa wanawake walio ktk ndoa,,wanawake 20 walisema wanapenda mume mpole ikiwa sifa ya 1 na 42 waliobaki waliitaja ikiwa ya 2
Huo ni utafiti binafsi ambao ulitaka kujua tu UPOLE WA MWANAUME una nafasi gani kwa mwanamke
Lakini kwa nini wanawake au mabinti hupenda mwanaume mpole? Kwa nini mkorofi hatajwi kabisa? Je ni kweli ni watu wanaohitaji huruma kiasi hicho? Mtaalamu wa masuala wa mahusiano wa kimarekani Baruck Miller aliyetafiti mahusiano kwa miaka zaidi ya 20,,anasema "... Mwanamke anampenda mwanaume mpole ili AJITAWALE KTK MAHUSIANO..."
Siku zote,mwanamke anapenda awe huru kwenda apendapo au kupewa atakacho.Hivyo anapokuwa mbele ya mwanaume mpole hana wasi,,wala hana tabu ya kutimiziwa shida yake.Akikutana na mwanaume mpole sana kiasi cha kukaribia ujinga basi atamuendesha mume/mpenzi kama rimoti control.
Jambo wanalosahau wanawake ni kuwa,,upole wa wanaume wengi wanautafsiri kama ujinga,uzezeta au kuliona kundi hili la kuchuna wapendavyo.
Laiti wangekumbuka kuwa mwanaume mpole ni kama volcano tuli,,ikilipuka imelipuka basi sifa ya upole ingekuwa ya mwisho.
Tags:
burudani ,
mapenzi

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “WANAWAKE WENGI HUPENDA WANAUME WAPOLE KWA SABABU HII”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.