Sunday, December 15, 2013

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MWANZA AUWAWA KWA KUPIGWA MAWE.




Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini Mwanza.

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wananchi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani? 

Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani. Kwa mujibu wa Katibu wa CCM ndg Joyce Masunga (maarufu kama Maziwa Fresh) ni kweli kuwa tukio hili limetokea na tunaendelea kufuatilia kupata habari zaidi.

Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kushambuliwa 


Mwili wa Aliyekuwa Mwenyekiti CCM wa mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Mhe. Clement Mabina baada ya kufikishwa hospitali ya rufaa Bungando

Tags: ,

0 Responses to “ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MWANZA AUWAWA KWA KUPIGWA MAWE.”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI