Tuesday, December 3, 2013
OFISI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YABAINIKA KUFANYA UFISADI WA SH BILION 23
Tuesday, December 3, 2013 by Unknown
Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) imeingia kwenye kashfa ya ufisadi wa Sh2.3 mil za Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali baada ya viongozi wa CCM wilaya hiyo kuitaja waziwazi kwamba wanahusika katika kashfa hiyo ilitokea mwaka 2011/12.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo alimweleza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliyetembelea wilaya hiyo jana kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ni moja ya kikwazo kitakachosababisha CCM iwe na hali ngumu wilayani humu kutokana na kuchelewesha kuchukua hatua za wahusika wa ufisadi huo.
Mwangomo alisema zipo dalili kwamba fedha hizo zilichakachuliwa kwa ushirikiano wa viongozi waliokuwapo mwaka huo na kwamba mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa.
Suala la ufisadi Mbarali liliitikisa halmashauri hiyo kwani madiwani sita walishahojiwa kwenye kamati ya maadili ya CCM kwa tuhuma za kushirikiana na watendaji katika kutafuna fedha hizo
Alisema hoja zote zilizotolewa atazifuatilia kwa karibnu na kwamba lazima zitatuliwe kabla ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani.
CREDIT : Mwananchi
Tags:
kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “OFISI YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YABAINIKA KUFANYA UFISADI WA SH BILION 23”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.