Monday, December 2, 2013

RUSHWA SIO-KAA TAYARI KWA MUSIC SHOW YA NGUVU PALE ARUSHA VIWANJA VYA GENERAL TYRE 7/12/2013






Afrika ni bara lenye wingi wa rasilimali. Na ni kutokana na wingi huu wa rasilimali bara hili limekuwa ni

chanzo cha rasilimali kwa bara lenyewe, mabara mengine na ulimwengu wote kwa ujumla kwa miaka,

miongo , na karni nyingi zilizopita. Raslimali mali hizi haziishii kwenye madini na malighafi nyingine, bali

pia zipo katika rasilimali watu na vipaji mbali mbali walivyokuwa navyo.

Katika vipaji vyetu, moja ambayo imekuwa ikitumika kwa karne nyingi hapa afrika kiasi tunaweza

kusema ni katika asili yetu , ni ile tutakayo zungumzia hivi punde.

muziki upo katika asili ya waafrika.na umekuwa ukitumika kuburudisha lakini zaidi kufikisha ujumbe

wenye kujenga na kurekebisha jamii hadhira. Iwe ni nyimbo, kughani amabayo hivi leo tunatambua kwa

jina la RAP, au hata iwe katika ala za vyombo mbali mbali kama marimba, ngoma na kadhalika.

Ni katika nyimbo ujumbe unahifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo, na ni katika nyimbo ujumbe

unafikishwa kwa jamii iliyopo huku ukiwaburudisha ili walengwa walazimike kusikiliza ujumbe kwa hiari

Sisi wana Meggamark entertainment, tukishirikiana na wadau AUABC na PCCB tuko hapo.

Dhumuni letu ni kutumia sanaa hizi ambazo zinaonekana kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa mkupuo

kufikisha ujumbe ambao tunaamini una manufaa si tu kwa walengwa wa awali, bali pia kwa walengwa

wa vizazi vijavyo katika bara zima la afrika.

Tunaamini kwa kwa kufanya hivi tunayo nafasi ya kufikisha ujumbe kwa namna ambayo ujumbe huo

unapokelewa, na zaidi kubebewa na wananchi na wengine wote wenye kufikiwa.

Kwa mantiki hii, tumeandaa onyesho lenye anuani isemayo “rushwa sio” ikimaanisha rushwa haina

manufaa na ni yenye kutakiwa kupigwa vita kwa gharama yoyote ile. Onyesho hili litafanyika Arusha

tarehe 7 mwezi wa kumi na mbili mwaka huu katika viwanja vya General Tyre kuanzia saa saba na nusu

mchana mpaka saa moja na nusu jioni. Litahusisha wasanii wenye kukubalika na jamii kubebea ujumbe

huu ili uweze kufikishwa kwa wananchi tukitegemea matokea mazuri yenye manufaa kwa wasikilizaji,

wananchi wa Tanzania, na bara zima la afrika kwa ujumla. Kati ya wasanii watakaoshiriki ni pamoja

na Fid Q, Chindo, Izzo Business, ROMA, Naziz (kutoka Kenya), Vanessa Mdee, Linah, Stamina,

na kundi la Weusi lionaloundwa na Joh Makini, Niki Wa Pili, G-Nako, na Lord Eyes. Wasanii

wengine ni pamoja na Mama C, Lumumba Band, Mo Plus, Frost, Fido, Kekuu, Bu-Nako, Jambo

Squad, Dogo Janja, Chaba and P-Culture. Tamasha hili litawapa nafasi pia wasanii mbali mbali

Tunaomba ushirikiano wenu katika hili , tukiamini mapambano dhidi ya rushwa ni jukumu la kila mmoja

wetu na ni kwa manufaa ya bara zima kwasababu sisi ni afrika, na afrika ndio sisi.

Tags:

0 Responses to “RUSHWA SIO-KAA TAYARI KWA MUSIC SHOW YA NGUVU PALE ARUSHA VIWANJA VYA GENERAL TYRE 7/12/2013”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI