Home
» kitaifa
» Baba amnyonga mwanae wa mwaka mmoja na kuacha ujumbe usemao: “Unyama unyamani,tutafute pesa kwanza niite j.m.k.a gaidi” Sakata zima soma hapa..
Tuesday, March 25, 2014
Baba amnyonga mwanae wa mwaka mmoja na kuacha ujumbe usemao: “Unyama unyamani,tutafute pesa kwanza niite j.m.k.a gaidi” Sakata zima soma hapa..
Tuesday, March 25, 2014 by Unknown
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya , Ahmed Msangi alisema jana mauaji hayo yalifanyika katika eneo la Migombani katika Mji mdogo wa Tunduma.
Alisema pembeni mwa mwili wa marehemu ulikutwa ujumbe unaosadikiwa kuandikwa na mtuhumiwa (baba wa mtoto) ukisomeka: Unyama, unyamani, tutafute pesa kwanza, niite J.M. a.k.a Gaidi.’
Alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo, ambaye Polisi inaendelea kumtafuta, ni Juma Venance ambaye umri wake haujafahamika.
Inadaiwa alifanya mauaji hayo Machi 22, mwaka huu saa 12, jioni na kisha alifunga mlango kwa nje akitumia kufuli na kutokomea kusikojulikana.
Kwa mujibu wa Kamanda, tetesi juu ya mauaji hayo zilipotolewa, maofisa wa Upelelezi wakishirikiana na raia wema walifika eneo hilo na kisha kuvunja mlango na ndipo wakakuta maiti ya mtoto akiwa amelazwa kitandani.
Kamanda Msangi alisema jitihada za kumtafuta mzazi huyo zinaendelea. Aliomba raia wema wenye taarifa za mahali alipo mtuhumiwa, wafikishe kwa kiongozi yeyote wa Serikali au kituo chochote cha Polisi cha jirani. Tags: kitaifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Baba amnyonga mwanae wa mwaka mmoja na kuacha ujumbe usemao: “Unyama unyamani,tutafute pesa kwanza niite j.m.k.a gaidi” Sakata zima soma hapa..”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.