Friday, June 21, 2013
Mtoto Afanyiwa Upasuaji Kuondoa Miguu Miwili Ya Ziada...
Friday, June 21, 2013 by Unknown
Mtoto Andrew Palismwe baada ya upasuaji huo.
Mtoto wa miezi miwili wa kiume nchini Namibia amefanyiwa upasuaji wa aina yake baada ya kuwa amezaliwa akiwa na miguu minne.
Andrew Palismwe, anayetokea Caprivi, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua masaa tisa kuondoa miguu miwili kwenye Hospitali ya watoto ya Red Cross War Memorial iliyoko mjini Cape Town, Afrika Kusini.
Mtoto huyo sasa anaendelea kupata nafuu kwenye Hospitali ya Windhoek Central nchini Namibia, imeripotiwa.
Alizaliwa akiwa na miguu miwili ya ziada chini ya tumbo lake Aprili 6. Hali hiyo inadhaniwa kuwa ni matokeo ya mapacha ambao hawakukamilika.
Daktari wa Hospitali ya Windhoek Central, Clarissa Pieper alisema: "Hii ni hali ambayo mapacha wameungana pamoja na kufuatia mimba ya mapacha ambayo hawakutengana kabisa, lakini kuunda watoto wawili wanaokua ndani ya kila mmoja. Katika suala hili, mtoto mwingine hauendelea kikamilifu."
Mama wa Andrew, Ruthy Mutanimiye alisema katika hospitali hiyo kwamba mtoto wake huyo wa kiume 'amepata nafuu haraka mara baada ya matibabu' baada ya siku nzima ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi.
Pia alizungumzia kuhusu faraja yake kwamba mtoto wake alifanyiwa upasuaji ambao asingeweza kumudu gharama zake.
Serikali ya Namibia ililipia gharama za upasuaji huo kupitia mfumo ambao husaidia wagonjwa wenye hali mbaya wasioweza kumudu gharama za hospitali binafsi.
Ester Paulus, msemaji wa Wizara ya Afya ya Namibia na Huduma za Jamii, alisema: "Mfuko huo ulianzishwa kusaidia wagoniwa ambao hawana njia yoyote kupata matibabu kwenye hospitali binafsi.
"Tunashughulikia kila ombi kwa uharaka, na kwa sasa, hakuna fomu zozote za maombi zinayosubiri kufanyiwa kazi."
Alikataa kutaja gharama za upasuaji wa Andrew, akisema: "Hakuna kiasi cha pesa kinachoweza kulinganishwa katika uokoaji maisha."
Tags:
kimataifa

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Mtoto Afanyiwa Upasuaji Kuondoa Miguu Miwili Ya Ziada... ”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.