Sunday, July 7, 2013

MBOWE AFANYA MAZUNGUMZO NA MAAFISA WA IKULU YA MAREKANI



Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye alialikwa kushiriki dhifa ya Kitaifa Ikulu wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani alifanya jambo kubwa muhimu kwa mustakabali wa Demokrasia hapa nchini.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Kiongozi Rasmi wa upinzani bungeni alipata fursa adhimu ya kufanya mazungumzo ya Faragha na maafisa wa Ikulu ya Marekani walioambatana na Rais Barack Obama.

Mpaka sasa kilichozungumzwa na Kiongozi huyo anayeongoza chama kinachopendwa na watanzania wengi zaidi hakijawekwa bayana ingawa wachunguzi wa mambo wanasema yalikuwa mazungumzo nyeti na muhimu kwa mustakabali wa demokrasia na amani ya Tanzania.

Taarifa zaidi zinasema Kiongozi huyo wa Upinzani nchini alialikwa na Ikulu kwa shinikizo kubwa kutoka ubalozi wa Marekani kutokana na Taifa hilo kutambua kazi kubwa inayofanywa na wabunge wa CHADEMA ndani ya bunge la Tanzania.

Tags: ,

0 Responses to “MBOWE AFANYA MAZUNGUMZO NA MAAFISA WA IKULU YA MAREKANI ”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI