Sunday, September 22, 2013

INASIKITISHA KENYA NA RAIA ZAO,TAZAMA HILI TUKIO LA KUSIKITISHA








Askari kanzu na mtutu wake mkononi akimuokoa mtoto na mwanamke kutoka eneo la tukio katika picha hii nadra ambayo inaeleza kila kitu.
Askari Kanzu akimuokoa mtoto
Askari kanzu wakitafuta magaidi chumbha hadi chumba
Askari kanzu na mtutu wake mkononi akishikilia tumbo baada ya kujeruhiwa
Watu wakitembea kwa magoti na mikono mbele ya mwenzao mmoja ambaye inaonesha ameshakufa



Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
--
KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya. 
Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shambulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.

Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi. 
Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali. 

Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia. 
Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo alifariki kutokana na majeraha yake. 

Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

Tags:

0 Responses to “INASIKITISHA KENYA NA RAIA ZAO,TAZAMA HILI TUKIO LA KUSIKITISHA”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI