Home
» kitaifa
» KUWA MAKINI: UTAPELI MWINGINE WAINGIA NCHINI; SASA WANATUMIA MITANDAO YA INTERNET YA KUOMBA AJIRA, TAFADHALI SOMA TAARIFA HII USIJE UKALIZWA
Sunday, October 20, 2013
KUWA MAKINI: UTAPELI MWINGINE WAINGIA NCHINI; SASA WANATUMIA MITANDAO YA INTERNET YA KUOMBA AJIRA, TAFADHALI SOMA TAARIFA HII USIJE UKALIZWA
Sunday, October 20, 2013 by Unknown
Kuna
UTAPELI mpya umeingia Nchini, kuna watu ambao wanajifanya wana
makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za
kazi, nafasi hizo za kazi huzitangaza kupitia mitandao ya Internet
ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja
mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna
mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo
ambayo tunaiongelea hapa.
Matukio yenyewe yanakuwaje: Watu hao hutangaza nafasi za kazi
mbali mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na
wanatafuta watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa
kutambua watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo
wanaamini wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la
Elimu na uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye
shida ya ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha
mawasiliano yako, wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na
kujifanya wao ni wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi
hiyo na kujidai wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka
uwatumie hela ili wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo
utaulizwa kwenye INTERVIEW na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida
ya Watanzania hawasemi wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha
Elfu kumi hadi Hamsini, wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira
unaweza ukakipata kiasi hicho.
Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao
utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo
ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana
haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha
ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu.
Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa
makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya
Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao
hiyo ujue ndio hao matapeli.
KUWA MAKINI EWE MTANZANIA
IMETOLEWA NA:
MDAU MPENDA HAKI
SOURCE;DJSEK
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “KUWA MAKINI: UTAPELI MWINGINE WAINGIA NCHINI; SASA WANATUMIA MITANDAO YA INTERNET YA KUOMBA AJIRA, TAFADHALI SOMA TAARIFA HII USIJE UKALIZWA”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.