Tuesday, October 8, 2013
WEMA, DIAMOND WAMTESA PENNY
Tuesday, October 8, 2013 by Unknown
ISHU ya wapenzi zilipendwa, Wema Isaac Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kurudiana inadaiwa kumtesa mpenzi wa sasa wa Diamond ambaye ni mtangazaji wa DTV, VJ Penniel Mungilwa ‘Penny’ hivyo kulazimika kukiri kuwa hajawahi kupitia wakati mgumu kama anaopitia sasa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na Penny, mwanadada huyo amekuwa akikosa amani kila anaposikia habari za Wema kurudiana na Diamond hivyo kuwa katika wakati mgumu.
“Watu wanapomwambia au kumuuliza Penny habari za Diamond kurudiana na Wema amekuwa akiumia sema tu watu hawajui,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, baada ya taarifa hizo kuwa habari ya mjini, mwishoni mwa wiki iliyopita, Penny alifunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anachokifanya ni kuhakikisha anamshikilia staa huyo wa Bongo Fleva hadi hapo Mungu atakapoamua vingine.
“Katika uhusiano niliowahi kuwa nao huu ni mgumu mno,” ilisomeka sehemu ya utetezi wa Penny aliouandika juu ya penzi lake na Diamond.
Hakuishia hapo kwani aliendelea kujitetea kwa wadau wake ambao walimjibu kuwa kinachoonekana anamhofia Wema ambaye akikita penzi lake kwa Diamond, kwa ustaa wake, atamfanya mwanamuziki huyo kuendelea kuliweka juu jina lake.
Katika maelezo yake, Penny alikiri kuwa mapenzi yanatesa lakini anaamini mateso hayo ni ya muda tu hivyo liwalo na liwe yeye anampenda Diamond.
Wiki iliyopita, Wema na Diamond waliripotiwa wakidaiwa kurejesha upya penzi lao lililozimika mwaka jana, jambo ambalo lilimpa Penny wakati mgumu huku akieleza kuwa anachoamini ni kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa penzi hilo.
Source:Globalpublishers
Tags:
burudani ,
udaku

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “WEMA, DIAMOND WAMTESA PENNY”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.