Monday, December 9, 2013
WASICHANA HAWA WAGUNDUA GENERATOR LINALOTUMIA MKOJO, WACHEKI HAPA
Monday, December 9, 2013 by Unknown
WASICHANA
wanne kutoka Nigeria wamegundua jinsi ambacyo mkojo unaweza kutumika
kama mafuta ya kusukuma jenereta. Wasichana hao, Duro-Aina
Adebola,Akindele Abiola, Faleke Oluwatoyin na Bello Eniola, wote wenye
umri wa miaka 14 wamefanya maonyesho ya jenereta hilo na limeonekana kufanya kazi.
Genereta
hilo linaweza kufanya kazi kwa muda wa saa moja likitumia lita moja tu
ya mkojo. Linauwezo wa kuendesha vifaa vinavyotumia umeme wa kati kama
vile taa, jokofu, redio, televisheni n.k, Sasa genereta hilo linafanyaje
kazi?
Kwanza mkojo huo unawekwa kwenye chombo kiitwacho
electolytic cell, ambacho hutenganisha mkojo huo na hydrogen. Kisha
hydrogen hiyo huenda moja kwa moja kwenye chujio la maji kwaajili ya
kuisafisha na kisha kuisukuma katika gas cylinder.
Hiyo gas
cylinder nayo huisukuma hydrogen mpaka katika kitu kinachoitwa, liquid
borax ambayo huisukuma hewa hiyo na kuliwezesha jenereta kufanya kazi.

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


0 Responses to “WASICHANA HAWA WAGUNDUA GENERATOR LINALOTUMIA MKOJO, WACHEKI HAPA”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.