Home
» mapenzi
» JEURI YA PESA...NJEMBA YAPORWA MKE NA MFANYABIASHARA....! JAPO INA SIKITISHA SANA! SOMA NA TAZAMA ZAIDI HAPA
Saturday, March 29, 2014
JEURI YA PESA...NJEMBA YAPORWA MKE NA MFANYABIASHARA....! JAPO INA SIKITISHA SANA! SOMA NA TAZAMA ZAIDI HAPA
Saturday, March 29, 2014 by Unknown

Kigogo wa kampuni ya kuchimba madini ya Afgem iliyopo Mererani mkoani Manyara, Abdallah Mwakaleja ‘Dullah’ anayedaiwa kupora mke wa mtu.
KIGOGO wa kampuni ya kuchimba madini ya Afgem iliyopo Mererani mkoani Manyara, Abdallah Mwakaleja ‘Dullah’ (38) anadaiwa kupora mke wa mtu, Violet Herman Masawe (29) huku ikisemekana anatumia jeuri ya fedha kumnyanyasa mwenye mke.
Akizungumza na gazeti hili, mume wa mwanamke huyo, Silvester Masawe mkazi wa Usa- River, Arumeru, Arusha alisema kuwa alifunga ndoa na Violet mwaka 2004 katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kalori, Usa River na kufanikiwa kupata mtoto wa kiume, Clinton Masawe (9).

Mlalamikaji huyo alisema baada ya muda mkewe alibadilika tabia na kuanza dharau na kutomheshimu mumewe.
Alisema aliamua kufanya uchunguzi wa kina na kubaini kwamba mkewe huyo ana uhusiano ya kimapenzi nje ya ndoa. Hata hivyo, Masawe hakuweza kufahamu nani anayeingilia ndoa yake kwa kupindi hicho.

Alisema hali hiyo ilimfanya awe mnyonge huku mkewe akifanya atakavyo, ikiwemo kuondoka nyumbani na kurudi muda anaotaka akiwa na harufu ya pombe hali iliyomlazimu Masawe kuishi kama mkimbizi ndani ya nyumba yake.

Hata hivyo, hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa kuwa mkewe hayupo nyumbani kitambo na baadhi ya bidhaa za dukani zimeyeyuka.
‘’Nilianza uchunguzi, ndipo nilipopata taarifa kuwa mke wangu anaishi na mwanaume aliyetajwa kwa jina la Dr.Dril (Dullah),” alisema na kuongeza:
‘’Niliamua kufuatilia ila sikuelewa walipokuwa wanaishi, lakini nilibahatika kupata namba zake za simu na kumpigia. Alinijibu hanijui na nikitaka nikashitaki popote kwani anayo fedha na kwa vile mwanamke nilimtelekeza, nimemwona amependeza, namtaka, simpati ng’o.”
Alisema alikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Usa River juu ya upotevu wa familia yake ambayo ni mke na mtoto huku akimtaja anayemhisi.
Mwanaume huyo alisema polisi walimpigia simu Dullah na alifika kituoni. Alipoulizwa kuhusu kuishi na mke wa mtu wakati akijua ni kinyume cha sheria, alikiri na kusema alikuwa hajui kama mwanamke huyo ni mke wa mtu. Polisi walimuamuru kumrudisha mwanamke huyo kwa mumewe, lakini hadi sasa hajafanya hivyo.
Akizungumzia tuhuma hizo alipoongea na gazeti hili, Dullah
alikiri kuishi na Violet na kujinasibu kuwa mwanaume huyo hana hadhi ya kuishi na mwanamke mrembo kama huyo kwani akiwa kwake alimchakaza ila kwa sasa amenawiri.
‘’Huyo mwanaume alimtelekeza mke wake kwa muda mrefu, niliamua kuishi naye kama mke baada ya kumwona ana sifa zote,’’ alisema Dullah.
Alisisitiza kuwa, hana mpango wa kumwacha mwanamke huyo kwa vile ameshamnunulia gari aina ya Toyota Noah kwa ajili ya kutembelea tu. Kwa upande wake Violet, alisema hana mpango wowote wa kurudi kwa Masawe kwani kwa sasa ameanza maisha mapya na kilichobaki anafanya mpango wa kupata talaka ndani ya mwezi huu.
GPL SOURCE. Tags: mapenzi

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
- JEURI YA PESA...NJEMBA YAPORWA MKE NA MFANYABIASHARA....! JAPO INA SIKITISHA SANA! SOMA NA TAZAMA ZAIDI HAPA
- Kwa nini Mwanamke Akishazalishwa Anakuwa Mwepesi Kuchukulika? SOMA ZAID HAPA....NA UTOE COMMENTZAKO
- TUKIO LILILO SHANGAZA ABIRIA KWENYE NDEGE, JAMAA AFANYA NG0NO YA MDOMO 0RAL S3X NA DEMU WAKE NDANI YA NDEGE TUKIO KWA PICHA NA STORI CHECK HAPA
- WANAO TEMBEA NJE YA NDOA NI MATAAHIRA NA WANA IQ NDOGO
- MWANAUME UKITAKA KUWEKA HESHIMA KWA MPENZI WAKO FANYA HAYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JEURI YA PESA...NJEMBA YAPORWA MKE NA MFANYABIASHARA....! JAPO INA SIKITISHA SANA! SOMA NA TAZAMA ZAIDI HAPA”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.