Thursday, March 27, 2014
SNURA"NITAPUNGUZA VIUNO KATIKA VIDEO ZANGU ILA KWENYE SHOW NITAZIDISHA MAUNO"
Thursday, March 27, 2014 by Unknown
Mwimbaji wa bongo flava ambaye pia ni muigizaji wa filamu za kitanzania, Snura amesema kuwa amepunguza viuno kwenye video za nyimbo zake kutokana na kukosolewa na hata kutolewa kwenye baadhi ya vipengele vya KTMA.
Akiongea katika kipindi cha Mitikisiko ya Pwani cha 100.5 Times Fm na Dida Shaibu, Snura ameeleza kuwa hata kabla BASATA hawajapiga stop ushiriki wa nyimbo zake kwenye kinyang’anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards alikuwa ameshabadilika kwa kuwa tayari video yake ya ‘Nimevurugwa’ ilikuwa imefungiwa.
“Tayari mimi nimeshabadilika kabla hata hatujafika huko kwenye Kili kwa sababu ilifungiwa muda kidogo kabla mambo ya Kili hayajaingia. Na wimbo wangu wa Ushaharibu nilikuwa nimeshafanya video pia, unajua nilikuwa nimeshafanya video ya Ushaharibu. Wimbo wangu wa Ushaharibu ukitoka watu watajua ni jinsi gani nimeweza ku-change.” Amesema Snura.
Ameeleza kuwa sio kwamba kwenye ‘Usiharibu’ hakutakuwa tena na uchazaji ule wa kukata viuno bali atapunguza kidogo.
“Kweli kwenye video sio kwamba hakuna kabisa kiuno ila nimepunguza. Nilichokifanya nimepunguza, nimeacha viuno ambavyo ninauhakika kwamba siwezi kufungiwa jamani. Sijakatika kama kwenye Nimevurugwa. Wakati nafanya wimbo wa Nimevurugwa sikuhisi kama naweza nikafungiwa kiukweli. Laiti kama ningejua nisingeweza kufanya vile. Nilichukulia kama ni ubunifu na utundu wangu ndio maana nikafanya vile.” Snura ameeleza.
Hata hivyo, amedai kuwa kuna mashabiki wake ambao wangependa kuona anacheza kama alivyokuwa akicheza zamani hivyo ataendeleza mchezo huo kwenye shows zake atazofanya kwenye kumbi.
“Najua nina mashabiki wale ambao wanakuwa wanapenda sana viuno, naomba wanivumilie kwenye video hawataweza kuona viuno kama vile ambavyo wao wanavihitaji, watakutana tu na kiuno cha kawaida. Ila kwa wale ambao wanaoweza kufika kwenye show zangu…kwenye show naweza kujiachia kama kawaida.”
Amefafanua kuwa havitakuwa viuno vitakavyokiuka maadili ya kitanzania na kuongeza kuwa yeye binafsi hapendi kuonesha jinsi anavyoweza kukata viuno.
“Lakini toka naanza kwenye muziki, nimefanya research nisipokatika…unajua kuna show nafanya nimesimama, lakini mashabiki wanalalamika wanataka kunipiga ‘sio wewe yaani wewe sio Snura kabisa, tunataka miuno’. Mimi nimfanya biashara sina jinsi inabidi nikatike ili niwafurahishe wateja wangu ili waweze kujaa kwenye show ili waweze kuingia kwenye show ili waweze kunikubali..mimi natafuta riziki.
Tags:
burudani

This post was written by: Author Name
Author description goes here. Author description goes here. Follow him on Twitter
Get Updates
Subscribe to our e-mail newsletter to receive updates.
Related Articles
- KANGA MOKO, VIGODORO NA T-SHIRT NDEMBENDEMBE VYAOIGWA MARUFUKU MISS TANZANIA
- BABU YANGU WEEE!! WEMA SEPETU PRESHA INA PANDA NA KUSHUKA, KUMBE DIAMOND HAJAACHA TABIA YA KUCHEAT, SASA ANATOKA NA KIMADA MWINGINE,,,,TAARIFA TOKA TIMU UKWELI NA UWAZI TUNAYO...SOMA NA TAZAMA PICHAZ ZA KIMADA HAPA
- SNURA"NITAPUNGUZA VIUNO KATIKA VIDEO ZANGU ILA KWENYE SHOW NITAZIDISHA MAUNO"
- TAZAMA VIDEO ILIYOIMBWA YA WIMBO ULIYOIMBWA NA WASANII ZAIDI YA 19 WA AFRIKA, AKIWEMO DIAMOND. D-BANJ, FALLY IPUPA....!!
- NAHISI ANA MWANAMKE ZAIDI YANGU..NATAKA NIMFUMANIE KWA SUPRISE VISIT KWAKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SNURA"NITAPUNGUZA VIUNO KATIKA VIDEO ZANGU ILA KWENYE SHOW NITAZIDISHA MAUNO"”
Post a Comment
Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.