Thursday, November 21, 2013

HII NDIYO TAARIFA NYINGINE KUTOKA KWA TANESCO KUHUSU MGAO WA UMEME UNAOENDELEA NCHINI KWA SASA!!



Dar es Salaam,Tanzania

WAKATI watanzania akiendelea kuteswa na mgao wa umeme, uliotokana na matengenezo katika mitambo ya kusafisha gasi kupeleka katika mitambo ya Shirika la Kusambaza Umeme Tanzania,(Tanesco),Mkurugenzi wa Shirika hilo Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kwamba, ukali wa mgao huo utaanza kupungua leo usiku baada ya mafundi wanaoshugulikia mitambo hiyo kukamilisha kazi yao kwa asilimia 80 ndani ya siku tano kati ya 10 zilizotangazwa awali.




Mkurugenzi wa Tanesco Mhandisi,Felchasmi Mramba akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Badra Masoud


Akizungumza na paparazi jijini Dar es Salaam,Mhandisi Mramba alisema kwamba, awali walitegemea kwamba kazi hiyo itakamilika ndani ya siku 10 zilizotangazwa awali, lakini kutokana mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani siku tano za mgao huo, wameamua kupunguza muda wa mgao na kwamba hali hiyo itaanza kuonekana leo.

"Awali tulitarajia kwamba kazi hiyo ingekamilika ndani ya siku 10, kama tulivyo tangazwa awali lakini kutokana jitihada za mafundi wanaoshugulikia suala hilo kuzaa matunda ndani ya siku tano, tumeamua kuwatangazia wananchi kwamba makali ya mgao huo utanza kupungua nguvu leo jioni"alisema Mhandisi Mramba.

Tags:

0 Responses to “HII NDIYO TAARIFA NYINGINE KUTOKA KWA TANESCO KUHUSU MGAO WA UMEME UNAOENDELEA NCHINI KWA SASA!!”

Post a Comment

Ila tafadhali sana angalia usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu.

HHHHHHHHHHHH

Subscribe

Kwa habari na Taarifa weka Email yako Hapa tutakutumia

© 2014 FUNUNU HABARI.. All rights reserved.
Designed by FUNUNU HABARI